EN SW

Sisi ni nani

Bayport ni Taasisi ya kifedha isiyo ya kibenki inayoongoza katita utowaji wa mikopo barani Africa na Amerika ya kusini .imeanzishwa mwaka 2001, na umiliki wake ukiwa Mauritius.

Taasisi ya Kifedha ya Bayport inatoa huduma zake katika Nchi zifuatazo: Botswana, Colombia, Ghana, Mozambique, Tanzania, South Africa, Uganda, Zambia na sasa Mexico. Kundi ya Bayport imetoa huduma kwa zaidi ya wateja 320,000 kupitia matawi yake 235 na zaidi ya wafanyakazi 2,500.

Bayport Tanzania ilianzishwa mwaka 2006 na kwa kasi imekuwa taasisi inayo ongoza katika utoaji wa mikopo kwa watumishi wa serikali na wafanyakazi wa makampuni binafsi yaliyoidhinishwa na Bayport nchini Tanzania. Bayport ipo katika mikoa yote Tanzania Bara ikiwa na zaidi ya matawi 83 na bado ikiendelea kukua.

Bayport inawezesha wateja wake kupata mtaji kwa haraka na Ufanisi, mara nyingi mikopo hii inapatikana katika muda mfupi, ndani ya masaa 24 baada kuidhinishwa.

Tunachofanya

Kwa kutoa mikopo nafuu, yenye sababu maalum, bila dhamana au amana, Bayport inajitahidi kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na kujenga maendeleo ya mtu binafsi. Kwa misingi hii wateja wa Bayport wamefaidika na wanaendelea kufaidika sana kutokana na mafanikio haya makubwa.